DRC - BARAKA/ FIZI:
Vijana wa Baraka watakiwa kujiepusha na hotba za uchochezi wa chuki za ubaguzi wa kikabila. Hayo ni kwa mujiba wa kiongozi wa Baraza la vijana wa mjini Baraka ABAHENYA Patient Rafiki katika maadhimisho ya siku kuu ya Vijana ulimwenguni akiwa katika ukumbi wa Meladen Club mjini Baraka siku ya jumamosi tare 12 Agoust 2023.
Message du Gouverneur de la province du Nord Kivu pour la population de la ville de Goma
RDCONGO: Kivu Kusini/ Vita vya M23 dhidi ya serikali ya Congo.
MKUU WA SHIRIKA LA RAÏA CHUMVI YA CONGO AWATAKA RAÏA WA MJI WA BARAKA NA TARAFA LA FIZI KUITIKIA WITO WA MAANDAMANO YA KULAANI UVAMIZI WA RWANDA DHIDI DRC KUPITIA M23./ by Madiba Mahoye
""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""
Mwenyekiti wa shirika la raïa NDSCI _ Chumvi ya Congo, limeitisha mkutano na waandishi wa habari wa radio na télévision, zinazo fanyia kazi katika mji wa Baraka na tarafa la Fizi, jumanne hii tare 08 Novemba 2022, kwa malengo ya kuipongeza kauli ya raïsi Félix Tshisekedi Tshilombo kwa kuwataka vijana kujiunga na jeshi la Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ili kupambana na quasi wa M23. Bwana Lusambya Wa Numbi katika.mazungumzo na waandishi wa habari amelaani kitendo cha nchi za Rwanda na Uganda kuivamia DRC kwa kujificha nyuma ya mgongo wa uasi wa M23.
Kiongozi hyo wa hasasi ya kiraïa amepatia fursa ya kutowa wito kwa vijana, kwa upekee pia na kwa raïa wote wakongomani kwa ujumla kuliunga mkono jeshi la Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa kazi ambayo jeshi hilo linayo fanya kwa kupambana na waasi wa M23. Lusambya Wa Numbe ameomba raïa wote wa Fizi na Baraka kuitikia kwa wingi katika maandamana ya kupinga uvamizi wa Rwanda na Uganda dhidi DRC, maandamano ambayo yanataraji kufantika siku ya numamosi tarehe 12 mwezi huu wa Novemba 2022.
Mwenyekiti huyo wa shirika la raïa bwana Lusambya Wa Numbe ameendelea kutowa wito kwa raïa wote kuitikia kwa wingi maandamano hayo na kuwaomba vijana kwenda kujiorozesha jeshini kwa wingi ili kuwafyeka waasi wa M23.